Swahili – Maombi Toka Dawati la Wanawake Machi

Februari inakuja na mabadiliko kadhaa kwenye Dawati la Wanawake la Umoja wa Ndugu- Kanisa la Moravian. Na hivyo tunawaomba ndugu wote, kote, kuomba Mungu aendelee kuongoza juhudi endelevu za dawati letu, kusimama pamoja na Dada zetu duniani kote na kusaidiana kama wapendwa na viungo imara vya mwili wa Kristo

Endelea kuinua maombi ya shukrani kwa uongozi wa Mratibu Mwanzilishi Mchungaji Patricia Garner na Wajumbe wa Halmashauri, dada Angelene Swart na dada Sallie Greenfield. Kwenye kikao chetu cha tarehe 31 Januari, 2019, dada Julie Tomberlin alisimikwa kuwa Mratibu wetu mpya; Bishop Blair Couch na dada Rachel Lwali walisimikwa kuwa Wajumbe wa Halmashauri  ya Dawati la Wanawake duniani. Hawa wanaungana na wajumbe wanaoendelea, dada Erdmute Frank na dada Muriel Held. Dada Liz Venable alichaguliwa kuwa Katibu na dada Jean Richardson kuwa Mtunza Hazina. Tuendelee kuwainua mbele za Bwana kwa maombi dada zetu hawa katika utumishi wao wa kuratibu maombi na majibu kadri ya mahitaji na matumaini ya wanawake wa Ki Moravian duniani kote.

Omba kwa ajili ya Makatibu wa Idara ya Wanawake wa majimbo yote duniani. Dada zetu hawa wanafanya kazi kubwa kwa niaba ya Dawati la Wanawake Duniani (UWD). Makatibu hawa ndio wanaokutana na wanawake na wasichana wahitaji bayana (uso kwa uso). Hawa ndio wanaelekeza jinsi ya kutuma maombi, kujaza fomu, kutengeneza mpango kazi wa miradi ili kuinua maisha yao, familia zao, Kanisa na jamii kwa ujumla. Kama humfahamu Katibu wako, wasiliana na dawati kwa tovuti: Unitywomen2011@gmail.com.

Omba kwa ajili ya Waratibu wasaidizi (Sub-Desk Coordinators), kwa kuwasaidia Makatibu wa Idara ya Wanawake wa Majimbo na kuisaidia Halmashauri  kutafuta njinsi ya kusaidia wanawake na wasichana wahitaji.

Omba kwa ajili ya shule za Kanisa la Moravian kote. Kwa wasichana watakaosoma katika shule hizi. Omba kwa ajili ya shule yetu mpya huko Ifakara, Tanzania iitwayo: PREISWERK GIRLS SECONDARY SCHOOL. Shule itafunguliwa tarehe 7 Januari, 2019. Omba kwa ajili ya uongozi wa shule, walimu na wanafunzi.

 Inua maombi ya shukrani kwa ajili ya jengo jipya kwenye shule ya MORAVIAN HERRNHUTER  ACADEMY – ZANZIBAR, Tanzania pamoja na watoto 220 wa chekechea  na shule ya msingi.

Tunapenda kuombea shule zote za Kanisa la Moravian popote zilipo pia shule zile ambazo kuna watoto wa ki Moravian wanasoma. ( Tuma jina la shule na picha za shule ili zipate kuombewa).

Omba kwa ajili ya wahanga wa moto kule Wuppertal, Afrika ya Kusini, walipatwa na janga hili  mnamo tarehe 30 Desemba, 2018. Waombee wale wote ambao biashara zao ziliteketezwa na moto, zimo pia zilizokuwa zinamilikiwa na dada zetu wa Moravian waweze kujijenga kwa upya.

Kanisa lione linawezaje kusaidia waathirika hao. Ndugu zetu Board of World Mission wa Marekani wanakusanya michango ya hisani kwa ajili ya wahanga.

Omba pia kwa ajili ya Cuba walioathiriwa na ‘tornado’ na kwa ajili ya wote waliothiriwa na majanga ya asili pote duniani.

Omba kwa ajili ya shirika zote ambazo kwa namna yo yote ile zinakumbwa na mitifuano mbali mbali ambayo inaathiri dada zetu na ndugu zetu ikiwemo Nicaragua, Honduras na Amerika. Mungu aingilie kati tofauti ziweze kumalizwa kwa upendo, uvumilivu na kuzingatia kweli hasa katika kumfuata Kristo.

Omba kwa ajili ya kambi ya Diakonia huko Paramaribo, Suriname. Hapa wanahudumiwa wahitaji toka pembezoni mwa nchi; kuna uhitaji mkubwa wa matengenezo ya miundombinu ili huduma iweze kutolewa kwa kiwango.

Omba pia kwa ajili ya wa Moravian wanaotoa huduma katika hospitali na kliniki kote duniani; pia wale wanaohudumiwa.

Omba kwa ajili ya wanawake na wakimbizi katika kambi ya UNHCR Dzaleka Malawi. Wanawake wa Moravian wa Ujerumani wamechagua kusaidia wakimbizi huko ikiwa ni mradi wao mkuu kwa mwaka 2019. Kanisa la Moravian Malawi wanaendesha mafunzo kwa wakimbizi hawa ya: afya, lishe, malezi, ukatili, kiingereza na ujasiliamali.

Omba kwa ajili ya wakunga huko Honduruas na Tanzania, ambao wamepokea ama watapokea zawadi za ‘birthing kits’ toka kwa wapendwa toka Ohio, NC, Florida. Bwana abariki huduma hii ya mama na mtoto.

Omba kwa ajili ya maandalizi ya Biennial Sinodi huko Jamaica Aprili 2019.

Omba kwa ajili ya tarehe 8 Machi, ambayo ni siku ya maombi kwa dunia nzima. Ombea wale wanaoandaa utaratibu wa maombi hayo.

Siku ya maombi ya dunia nzima ni 1 Machi, 2019. Panga kuungana na wanawake toka nchi 170 kutafakari neno toka injili ya LUKA MT. 14:15 – 24.

Utaratibu wa 2019, umeandaliwa na dada zetu wa Slovenia

Waombee dada zetu wanaoandaa mkutano wa 13 wa Moravian Women’s Conference huko Winston-Salem, NC June 20 – 23, 2019. Omba pia kwa ajili ya wale wanajiandaa kuhudhuria waweze kupata vibali vya kusafiria.

Tafadhali, tushirikishe ni jinsi gani tunaweza kuomba kwa ajili ya wanawake katika jamii yako na jimbo lako.

ENDELEA KUOMBEA DAWATI LA WANAWAKE DUNIANI